Mradi huu uliongozwa na Kanuni na Njia Kamili za Ufuatiliaji ikianza na njia mbili za awali za kuanzisha na kuunda program ya eCDT ambayo inaweza kuleta faida za kiikolojia, kijamii, na kiuchumi katika uvuvi wa pweza wa Tanzania. Mkakati huu unaelezea kwa kina mbinu zetu, hali ya sasa na changamoto za ufuatiliaji wa pweza katika Wilaya ya Kilwa, matamanio na vipaumbele vya baadaye kama ilivyoelezwa na wadau husika, na mapendekezo ya taarifa za ufuatiliaji. Mkakati huo una lengo la kutoa taarifa za hatua zinazofuata ili kuchochea hatua za kuunda na kutekeleza mpango wa eCDT kwa uvuvi wa pweza wa Wilaya ya Kilwa. Hatua hizi zinazoweza kutekelezwa zimeelezewa katika shughuli za mpango kazi ambazo zinakusudiwa kuongoza miezi 12 ijayo.
Bofya hapa kwa Kiingereza.